Tuesday, March 5, 2013

KONA YA MAPOCHOPOCHO'''by NANZA MBUJI

     Wadau ni kipengele kipya katika blogu yangu ambapo nitakua nikikuletea mapishi mbalimbali na kwa pamoja tunaweza kubadilishana ujuzi katika eneo hili la jikoni. Tunajua watu tuna ujuzi mwingi jikoni na kutokana na hilo basi tusiwe wachoyo kushirikiana katika kijieneo hiki ha haaaaaaaa'''.
Kupitia hapa nakukaribisha wewe mdau wangu unitumie aina la pishi uliloamua kutufundisha  katika eneo lolote yaweza kuwa ni vyakula vya kawaida vya watu wazima,matayarisho ya juyce mbalimbali,vyakula vya watoto,refreshments etc na tutaiweka hewani kwa faida ya wote,
tuma kupitia bkanemba@yahoo.com au tuwasiliane kwa 0714950054 na tutajie na jina kamili au ukipenda tupia na picha yako tujue nani aliyetuandalia,khaaaaa hii ni wonderfull

 

 PISHI LA MCHUZI WA KUKU WA NAZI NA MAYAI YA KUCHEMSHA







Vipimo
Kuku 2 Lb (ratili)
Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai
Ndimu 1 kamua maji
Chumvi kiasi
Bizari manjano ½ kijiko cha chai
Vitunguu maji 1
Nyanya 2
Tuwi la nazi zito 1 ½ kikombe
Mayai ya kuchemsha 6

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Mchemshe kuku na tangawizi na ndimu na chumvi mpaka akauke.
  2. Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika mashine (blender).
  3. Mimina kwenye kuku pamoja na bizari zote.
  4. Acha achemke kisha tia tui lichemke mpaka liwe zito
  5. Tia mayai ya kuchemsha.
  6. Pakua kwenye bakuli tayari kuliwa na wali au mkate 
   Shukrani za pekee zimwendee 
       Wa ukweeeel'''nanza mbuji
              BIG UP kwako na tunasubiri mambo mazuri   zaidi toka kwako.

 WADAU,kaeni mkao wa kula next tym ntapost picha zake,stay tuned''''
                                         
                   '' KHAAAAAAA'HAPANA CHEZEA YEYE''