Sunday, December 30, 2012

KID's beds designs PARTY 4


Tuliweka pazia, chumba chao kina madirisha 2....watoto ni wa kiume.....miaka yao ni wa kwanza ana 2 yrs. na wa pili ana miezi   3 sasa....



Kitanda hiki ni cha mtoto wa miezi 3, tulimuewekea hizi chuma pembeni ili kuzuia asidondoke....



vitanda vinavyoonekana kwa mbali......magodoro yatawekwa na yeye mteja, alikua hajanunua bado...

  Pazia kwa mbali na vitanda.... chumba kilipendeza .....

 

MWAKA 2013!!!!!!!! RUHUSU AMANI YAKE KATAA MAHANGAIKO


Yamebaki masaa machache mpaka kuuona mwaka 2013'''''

Jamani Mungu ana huruma, wema,neema,rehema,upendo sana,

ukitafakari unaweza anza kulia tu hata kama ni mwanaume na haijalishi uwe ofisini,maombini, unaendesha gari,umelala,unatembea, unapika,unasoma, unalima huko village, uko bafuni unakoga, unaweza piga magoti huko huko hata haisumbui, maji ya mvua uyayokoga yanapoendelea kukumiminikia, unaweza anza kububujika na machozi ya furaha na kunena mara tu ukumbukapo wema  na fadhili zake............


Usikate tamaa kwa yale ambayo hayakuwezekana 2012 basi amini kuwa yatafanyika kwa uwezo wake,.....

blogu hii ya burudika inawatakia kila la kheri katika maandalizi ya kuukaribisha mwaka 2013!!!!

WE ALL LOVE UUUUU!!!!!!

 

 

WANAMUZIKI WA INJILI NA WACHEZA FILAM WAKIWA NA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO

Ni kikao kikubwa kati ya wadau na viongozi mbalimbali wa muziki na filamu na Mheshimiwa Makala ambaye ni Naibu waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo

Lengo la kikao hicho ni wasanii kufahamishwa jinsi serikali ilivyojipanga kuwasaidia wasanii wa Tanzania, ili wanufaike na kazi zao na kuwajengea heshima zaidi.

Katika kikao hicho chama cha muziki wa Injili Kimewakilishwa na  Addo November, John Shabani, Bahati Bukuku, Upendo Kilahiro, Cosmas Chidumule, George Mpella na Stella Joel,pichani ni matukio katika kikao hicho




              Bahati bukuku akiongea jambo wakati wa kikao


        Hapa wadau wakipata picha ya pamoja wakati wa kikao hicho


            Pichani ni mcheza filamu maarufu JB akichangia hoja na mawazo yake

        



            Ni mcheza filamu Ray akiongea na waziri wakati wa kikao hicho