Sofa Repair.....
Kuna mdau alinituma swali, kua kama anataka kubadilisha sofa kitambaa inawezekana?
Jibu ni kua, kwanza tuione hiyo sofa, na pia inategemea na uchakavu
wake. maana kuna zingine zimechakaa mpaka zile mbao za ndai zimevunji.
sasa kwa sofa ya aina hiyo hua nina shauri ununue ingine...maana
ukarabati wake utakua ni mkubwa, tena karibu sawa na kua sofa mpya....
Naomba ndugu wadau, muwe mnanitumia picha ya sofa zenu ili niweze
kuziona kabla ya kutoa jibu....nitumie email bkanemba@yahoo.com
AU Simu namba 0714950054
SOFA, BEFORE AND AFTER......
Sitting room ikiwa tayari imebadilika.....Homez Deco tuliweza
kuibadilisha sofa kidogo iweze kupata muonekano mwingine.....tuliweka
foronya za green, cream na animal print.....Color ya sofa ni dark
brown.....
Hapa sofa ikiwa bado haijabadilika muonekano.....
This was Furnitures 4 Sale....
Mnaikumbuka hii set, ina 3 sitter 1, 2 sitter 1 na single sitter 1....
na hii aliyokalia hapa ilikua ni oda ya mteja
After........Living room transformation @ Tabata.......(Tunakushukuru mteja wetu wa Tabata.... )
Sina
mengi ya kuongea...sofa ni L-shape na 2 sitter moja ila kila kitu kina
wezekana ukijipanga, hapa tumeanza na sofa.... tutakuja mapazia, then
decorations...... ambapo rangi hii ya sofa, inakubali kutupia pillows,
na throws color yoyote ile........
Mbao tunazo, sponges zipo... etc,
Dunia ni yako, Chaguo ni lako...
(Ukiamua kuvaa, nyumba ikafuata,ama, ukiamua kutengeneza nyumba, then kuvaa kutafuataa.... uamuzi ni wako)
Haujachelewa kupanga ratiba ya nini cha kubadilisha nyumbani kwako......
Tuwasiliane, kwa ushauri, huduma zetu......
Regards
beatrice
NB:
Kazi hii ilichukua wiki moja na nusu,, na kama kawaida ya Homez Deco,,
tuna Time Frame..... Alipata muda tuliokubaliana........
L-shape metal sofa.....
Hii ndio sofa ya L-shape inavyoonekana na inavyokua ikiwa
tayari.....sasa inategemea wewe unapenda rangi gani za vitambaa
tukushonee kwa ajili ya covers.....
Upande wa kwanza wa L-shape
Upande wa pili wa L-shape
akiwa amepose baada ya ku set sofa.....hapa kazi tu kwakweli.
Ukifanya kazi nzuri, na mteja akaipenda, unakua na amani ......sylivia akiwa amepozi
Sofa
hii ya L-shape ni shs. 1 million..... usafiri ni juu ya mteja.....
tunachofanya sisi kuna gari ambalo tunalitumia mara kwa mara na ni
waaminiifu. sasa wakikuletea mzigo unalipa usafiri, na hii ninasaidia
ili msipate usumbufu wa kutafuta usafiri.......
Karibuni sana mtoe orders......
Kazi ya Homez Deco-Kreative Homez, Site- Mbezi Beach.....
Ni
vitanda vya four poster, design 2 tofauti, na wengi wenu mmekua na
maswali kua vitanda hivi vinakuaje na je kama ni imara, jibu ni kua
vitanda ni imara tena kuliko mbao, maana mbao asilimia kubwa zinaliwa na
wadudu;
Ukubwa wa vitanda hivi ni 4 by 6, na tumeweka godoro la 4 by 6 inch
8....(hatutoa karatasi za godoro maana bado kuna kazi
zinaendelea......yasichafuke) na godoro waweza kuweka lolote lile
kulingana na uwezo wako na kukapendeza.
YAAAAAAAANI NI KAZI KWAKWENDA MBELE''''
Mbezi Beach Project.....Iron furniture by Homez Deco.....
Asikuambie
mtu fanicha za chuma zinapendeza sana... na hautogombana na dada wa
kazi kua hafanyi usafi chini ya makochi......kote kunaonekana.....
Dinning table.......ya viti 5.....
Mto ukiwa na cusion cover na tayari kwenda kwa mteja...
Mto ukiwa na linning....
Kiti kikianza kuonyesha muelekeo....
Ninashukuru mungu kua sasa nimeweza kuwapatia vijana ajira hapa mtaani kwetu kwenye ofisi yangu........
Hapa nikikagua kazi, mito kama ujazo uko sawa na inakaaje kwenye kiti....kazi hazitoki mpaka nimezikagua.....
Hii
ndio kazi ya yale magodoro madogo madogo ambayo tuliyakata kata vipande
vidogo vidogo, tukavichanganya na fiber, na tukashona decron
tunazitumbukiza ndani mchanganyiko huo, na tunashonea lining, mwisho
tunashonea foronya ama cover, na mto unakua tayari.
Kama kawaida
yetu Homez Deco, hatufichi kitu, mito yetu ni imara na haina harufu hata
ukimwagia maji, utauanika na utakauka na hakuna harufu itakayotoka ama
kutoa alama kwenye mto....maana tunaweka vitu visafi tuuu..... mito ni
soft na inadumu kwa muda mrefu bila kusinyaa.....
Hii ndio ile
nyumba ambayo nilitengeneza curtain poles za chuma, vitanda vya chuma,
vya four posters, nikawaonyesha, na last week tukamaliza na meza ya
chakula na makochi..... wishing you all the best my dear
customers.......
Asante sana mteja wangu na zawadi yako ya magazine rack iko jikoni......nitawaonyesha......
Site ya Kigamboni.....Homez Deco tuliweka Kabati la nguo la Mninga....
Hili ndilo kabati languo la mninga muonekano wake wa nje.....mteja alihitaji kabati litakaloweza kuhifadhi nguo za watoto wa kike wa wili na kama atatokea mgeni basi nae anaweza akaweka nguo zake hapo....na wote waweze kuweka viatu....
Kabati muonekano wa ndani.....Kama unavyoona Kushoto na kulia kuna fanana, nikiwa na maana ya kwamba, kuna sehemu ya ku hang nguo, kuna sehemu ya ku kuweka nguo zilizokunjwa, na kuna droo mbili kila upande, na katikati ndio sehemu ambapo mgeni akija basi ana uwezo wa kuweka nguo hapo bila kusumbua wengine.....na chini ndio sehemu ya kuweka viatu....
Kama kawaida, pozi baada ya kazi ni muhimu baada ya kuikagua na kuridhika nayo....
ha haaaaaaaaaaa,so happy kwakweli
NB:
Mbao nzuri kwa makabati ni mninga, mkongo, kwa wale wanaojiweza...na kuna mbao zingine ambazo ni mpodo, etc.....Mbao ni gharama hasa kwa kipindi hiki ambacho miti haikatwi katwi ovyo.....
Mninga ama Mkongo, ni imara na hupendeza sana.....
Waweza pia kutengeneza kabati la nguo la MDF, ni haya makabati ya ready made.....ambayo tunayaona madukani....ila sio imara kwakweli, na hayataki shida, kama kuhama hama, etc...
Karibuni sana kwa mahitaji ya makabati ya nguo, ya jikoni, etc.....
Homez Deco tutakuja kupima nyumbani kwako ama sehemu utakayotaka tukuwekee...maana hatupokei vipimo vya mteja.....na kukupa bei kulingana na design, na mbao uliyoichagua.....
Kabati za ndani.... Mbao aina ya mninga....mbao zetu....
Jumapili ya juzi, nilikwenda site eneo la Goba....., lengo ni kwenda kupima pazia, na hii ni baada ya sisi kuweka curtain poles, kama kawaida yetu, jamani kizuri kisifie.....na chema chajiuza....
Nyumba hii ni nzuri, na nilipenda na nikamsifia sana mwenye nyumba, na ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuruhusu kupiga picha ili tuweze kushirikiana katika hili...
kuna msemo usemao, kizuri kula na nduguyo, na kibaya ........
Tulipenda kila kitu, yaani tiles, makabati etc.....
Tumeonelea tuangalie makabati haya na uniambie kua umeyaonaje,
kwa mtazamo wangu, fundi aliyeyatengeneza haya makabati anastahili sifa, maana haku chakachua, na finnishing yake ni nzuri. maana hata milango pia ni mninga......na fundi huyu hana usumbufu wa kazi.......
kwa mahitaji ya milango makabati wasiliana na fundi huyu
anaitwa fundi Dennis tunamshukuru tena mteja wetu huyu kwa kutupa mawasiliano ya huyu fundi ili wote tusingie hasara, maana mafundi asilimia kubwa ni kula hela za watu na kiswahili kingi....
ikawa hivi tena.......
Before & After Site ilikua Sinza......Curtains by Homez Deco....
NI handsome Jaydan, tunaanza kutembea sasa, usijiulize anafanya nini site.... hahhaha.... tunaanza kurithisha mapema.... hahhahahahh
Fixer baada ya kazi......
Mie naangalia kazi....hapo jayd yuko mbali.....
Curtain holder...
fixer akiwa kazini....
Wakianza ku fix
wakitayarisha pazia
kwa wale wenye curtain box, ni maranyingi hua tunaangalia hali ya reli. kama hazifai twabadilisha. hapa wakibadilisha....
before sitting room curtains make over.....
hapa kabla hatuja badilisha pazia....
Niliipenda hii decoration...
pazia zikishushwa...
hua kabla ya kuweka pazia mpya, kua tunafuta vumbi kwenye curtain poles...
pazia hizoooo kabla hatujazipandisha....
shee zikiwekwa kwanza...
zikipandishwa...
inafuata pazia, main curtain
hivi ndivyo inavyoonekana baada ya kurekebisha...
marinda yakiwekwa.......
hua tuna cheki kama pazia zimekaa vizuri....
baada ya kuweka pazia, hivi ndivyo muonekano mpya wa sitting room....
hii inaitwa puff, inaweza kukaa sitting room, ama chumbani, miguuni mwa kitanda....
hapo chachaaa......., pazia zako za zamani zaweza pata muonekano mpyaa......na zikapendeza....
kazi imekwisha....
Curtains before & after........ Kijichi Mgeninani.....kazi ya Homez Deco.....
Sitting room.........After...... sasa mteja wetu kabla ya kutengeneza pazia kwetu tulimshauri abadilishe rangi na apake, cream ama butterscotch, sasa kama ninavyosema jamani taratibu unaweza, mdau wetu huyu yeye alikubali kubadisha rangi, na akasema kua ataanza na mapazia, maana alikua na harusi, so angependa mapazia yawepo, jana ndio tumefunga pazia na leo ndio harusi, tunakutakia kila la kheri..........(RANGI YA UKUTA ITABADILISHWA NYUMBA NI MPYA NDIO WAMEHAMIA, TUTAWALETEA HUMU HUMU)..
Asikuambie mtu jamani, ukifanya kazi yako na ikapendeza na kutoka ontime, ni furaha ajabu... hii ndio team... mie hapo nilipumzika, kazi yangu ilikua kupiga picha.....haahaha.....
ninachompendea mafundi wetu yaani wanafanya kazi na anaipenda kazi yake... hakuna kuchanganyana, kazi kwa kwenda mbele....
fundi akiweka rail....
kwa wale wenye curtain poles, pls mkitaka decoration ama swag, pls weka rail kama inavyoonekana hapa, na sio kuweka chuma tatu..... haipendezi.....
Haya, kazi iko hapa, marinda yakitengenezwa... Phides alifanya kazi hiyo....jamani unajua bwana, hata kama ukiwa bosi katika biashara yako jitahidi uijue kazi yako, kwani itakusaidia sana na hautakua na stress hata chembe......good work Phides...
ukiipenda kazi yako na ku meet dead line.. siku zote ni furaha tuuu Phides weee naona smile lako.....
Vyote vinaenda kwa vipimo.... bila vipimo ni kazi bureeee
Wakiweka decoration, kwa kiutalamu inaitwa swag..(huu ni urembo wa juu)
Phides akimuelekeza fundi....
Phides & Fundi wakisaidiana ku fix pazia......
Dinning....
hii ni kabla hatujaweka pazia.....
Before & After (Curtains) Mbezi site....
Before & After House make over...(Tabata site)
Kazi imekwisha........Karibuni sana kwa mahitaji ya pazia, kubadilisha covers makochi, viti vya dinning, interior decorations, furniture arrangment, ushauri, kupaka rangi kuta, fanicha za chuma, Landscaping & gardening, interior design etc.......Ukifanya kazi yako kwa umakini, na upendo, kila kitu kitakwenda sawa.......Naipenda kazi yangu.......
Wallpaper, huu ukuta uliokaa tv, tunaita ni focal point, ya sitting room yetu, nitaja elezea nini maana ya focal point siku ingine...tuliweka wallpaper rangi ya offwhite, na ni wash able, ikichafuka unaifuta na maji kidogo...
Hapa tukivalisha cusion covers tulizozishona Homez Deco....
Hizi ni pazia za vyumbani, kama tunavyoonekana mzigoni, hakuna cha boss wala mfanyakazi, we work as a team work......
Maua haya niliyapenda sana.... ninamtafuta huyu anaefanya shughuli hii then nitawapa contacts zake kwa watakao muhitaji..... ni maua ya artficial...(yanafanana na ya kariakoo haya...)
Kiti cha kulia ndio kilichobadilishwa na fixer wetu....
Fixer akibadilisha cover za viti vya dinning.....
Tukianza kazi ya ku fix pazia za sitting room......
L-shape metal sofa.....
Hii ndio sofa ya L-shape inavyoonekana na inavyokua ikiwa tayari.....sasa inategemea wewe unapenda rangi gani za vitambaa tukushonee kwa ajili ya covers.....
Upande wa kwanza wa L-shape
Upande wa pili wa L-shape
Akiwa nimepose baada ya ku set sofa......
Ukifanya kazi nzuri, na mteja akaipenda, unakua na amani ......
Sofa hii ya L-shape ni shs. 1 million..... usafiri ni juu ya mteja..... ninachofanya mimi kuna gari ambalo tunalitumia mara kwa mara na ni waaminiifu. sasa wakikuletea mzigo unalipa usafiri, na hii ninasaidia ili msipate usumbufu wa kutafuta usafiri.......
Karibuni sana mtoe orders......
''''''STAY TUNED MORE GOOD THINGS TO COME GUYS''''''