EEEHHH' MUNGU tusaidieeee''
Siku hizi binadam tumekuwa kama wanyama NA ni afadhali na mara mia ya wanyama na hatuoni thamani tulizonazo hata kufanya yasiyostahili....Hii ni habari ya mda kdg ila katika pitapita zangu kuna rafiki yangu wa karibu alinipa hii ''case'' ya huyu dada jamani kwakweli binadam wa sasa ni wachache wenye huruma na utu.....kweli wapo ila sio wote ni wachache mnooooo,jamani mnooooo'''mh''nilishindwa kuvumilia chozi likanitoka
Kwa wewe ambae hukuona ilikua hivi,,,,
Sophia rashid
“HAYA ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si kazi ya binadamu, nasikitika
kwa sababu mume wangu amenitelekeza baada ya kuona watoto wamevimba
kichwa,” hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sophia Rashid , 22, mkazi wa
Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambaye anauguza wanaye
wawili wanaosumbuliwa na uvimbe wa kichwa.
Mama huyo alisema watoto wake hao aliwazaa wakiwa na matatizo ya kuvimba vichwa kutokana na kujaa maji, hali ambayo inamfanya akose raha.
“Kwangu sasa imekuwa ni matatizo makubwa mwanangu Omari mwenye miaka minne na Maulid mwenye miezi kumi wanasumbuliwa na ugonjwa mmoja ambao umesababisha baba yao kuwakimbia,” alisema mama huyo akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi)…

Aliongeza
kuwa, tangu alipofika hospitalini hapo wiki mbili zilizopita, amekuwa
akipata msaada kutoka kwa maofisa wa ustawi wa jamii wa Moi lakini ndugu
zake hawafiki kabisa kumjulia hali.
Daktari
mmoja hospitalini hapo aliyezungumza kwa sharti la kutoandikwa jina
gazetini alisema kuwa, hali hiyo huwapata watoto kutokana na kuwa na
upungufu wa madini ya pholic acid na mjamzito kukosa lishe bora wakati
wa ujauzito.
MSAADA
Kutokana
na matatizo hayo mama huyo anaomba kusaidiwa na mtu yeyote aliyeguswa
na masaibu yake kifedha, chakula, mavazi, dawa pamoja na kipimo cha TC
Scan ambacho alidai kuwa kipo katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar
es Salaam na gharama yake ni shilingi 258,000 kwa mtoto mmoja.
Atakayependa kumsaidia mama huyo atumie simu namba 0716755384 au afike Hospitali ya Muhimbili, Moi kwenye wodi A.