Sifa na utukufu ni kwa Mungu wetu aliye hai!
Neno la Mungu linasema,
Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; uendapo katika moto
hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.(Isaya 43:1b-2).
Mpendwa
kumbuka Mungu aliyekukomboa alikuahidi kuwa atakuwa pamoja nawe wakati
wote, kumbuka pia Mungu si mwanadamu hata aseme uongo. Simama imara
ukiliitia jina la Bwana, songa mbele ukimtumikia na kumtumainia hakika
hatma yako njema ya ushindi inakuja. Kwa maana Bwana anasema “…Iandike
njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma
kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya
haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia
INGOJEE kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia!(Hab.2:2-3).
Usikate tamaa
mpendwa, kumbuka ahadi za Bwana juu ya hali unayopitia, kiri ushindi kwa
kuwa wewe ni mshindi! unajua kwa nini…!unayemtegemea, Bwana Yesu
alishashinda pale msalabani!usife moyo, songa mbele. Mungu akubariki.
Hakika Mungu yeye anaishi na kamwe hapungukiwi,ni angela chibalonza na wimbo wake WA yahwe uhimidiwe,
Please sikiliza huu wimbo na utafakari