Friday, December 21, 2012

ALIYEDHANIWA AMEKUFA AFUNGA NDOA KANISANI

YAHWE UHIMIDIWE!!!!!!!!!! 
 Uaminifu wako umejulikanaaaaaaaa'''''''''
Kwa mataifa yote ya ulimwenguuu'''''''''
Yahweeeeeeee eeeeeeeee''''''''''''

Hakika shetani imekula kwake..........ilikua ni kwamba asiione siku yake inayofuata ila Mungu aliweza kujidhihirisha   miongoni mwa nguvu za giza...JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akimvisha pete mkewe Magreth Mtebe huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru Mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Jumamosi.







Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi Emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100  Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia Jumamosi mida ya saa sita na nusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndipo ajali hiyo ikatokea maeneo ya Mafiati Mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo.














Tuna kila sababu ya kukiri kuwa shetani ameshindwa na hana mamlaka katika ufalme wa Roho mtakatifu








NANI MSHAMBA YA STARA THOMAS

  STARA THOMAS.............                     


 Ni Aliyekua muimbaji wa nyimbo za bongo fleva Stara Thomas sasa amempa Bwana Yesu maisha yake!
 

Hapo awali alisikika kwa nyimbo maarufu kama Sikia, Sitorudi nyuma, my body na Chldren rights ambapo hivi karibuni amevuma na wimbo wa nipigie alioshirikishwa na AT.
 

Stara alipoulizwa kuhusu  maamuzi yake haya binafsi alieleza 

“Nilipata wito kutoka kwa Yesu kwa kuwa aliwaita watu wote wasumbukao na kulemewa na mizigo waende kwake atawapumzisha” alisema.


Awali alikua akiabudu dhehebu la Jamatrine kwa sasa anaabudu kanisa la Shalom lililoko Mbezi Salasala! NA endapo ukihitaji kumuunga mkono kwa kununua album yake mpigie simu ifuatayo +255 718 030 411


    Uongozi wa BURUDIKA BLOG UNAKUTAKIA KILA LA KHERI NA MUNGU AKUBARIKI katika kulitangaza jina la bwana


Hii ni cover ya Albamu yake hiyo mpya kama inavyojieleza
hapa ikionyesha nyimbo zilizomo katika albam hiyo
                    



VIONGOZI WA CHAMA CHA INJILI WAPATIKANA RASMI

Ni katika  Hotel ya Wanyama iliyoko Sinza Mori kumefanyika kongamano la waimbaji wa Muziki wa Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania "CHAMUTA" 
 limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania.

Katika kongamano hilo lilihudhuriwa na Mfuko wa pensheni wa LAPF.Mfuko huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae,pia kutoa fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.  

Pichani ni baadhi ya matukio katika kongamano hilo


Mwanamuziki mkongwe wa injili UPENDO KILAHIRO akiongea katika kongamano hilo katika Hoteli ya wanyama sinza


Mwimbaji wa muziki wa injili BAHATI BUKUKU akisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo



                           Mwimbaji mkongwe nchini mzee Makasy akiandika point muhimu

               Pastor Abel Orgenes ambaye amekuwa karibu sana na waimbaji wa gospel


                 Comedian King Chavala alikuwepo kujua umuhimu wa chama hicho

 Hapa ni mwimbaji maarufu Addo November Mwasongwe Rais wa chama cha wasanii akiwa na mkurugenzi wa Grace Product.

PICHANI CHINI............

           Abubakar Ndwaka meneja mafao wa LAPF akizungumza jambo katikakongamano hilo