Ni katika Hotel ya Wanyama iliyoko Sinza Mori kumefanyika kongamano la
waimbaji wa Muziki wa Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa
Injili Tanzania "CHAMUTA"
limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha
viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania.
Katika kongamano hilo lilihudhuriwa na Mfuko wa pensheni wa LAPF.Mfuko
huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao
kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae,pia kutoa
fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya
baadae.
Pichani ni baadhi ya matukio katika kongamano hilo
Mwanamuziki mkongwe wa injili UPENDO KILAHIRO akiongea katika kongamano hilo katika Hoteli ya wanyama sinza
Mwimbaji wa muziki wa injili BAHATI BUKUKU akisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo
Mwimbaji mkongwe nchini mzee Makasy akiandika point muhimu
Pastor Abel Orgenes ambaye amekuwa karibu sana na waimbaji wa gospel
Comedian King Chavala alikuwepo kujua umuhimu wa chama hicho
Hapa ni mwimbaji maarufu Addo November Mwasongwe Rais wa chama cha wasanii akiwa na mkurugenzi wa Grace Product.
PICHANI CHINI............
Abubakar Ndwaka meneja mafao wa LAPF akizungumza jambo katikakongamano hilo
No comments:
Post a Comment