Monday, March 25, 2013



HONGERA SANA NANCY (MAMA ZURI) KWA KUTOA KITABU KIZURI CHA WATOTO,HILI NI WAZO ZURI KEEP IT UP'''''
 

 ni miss tanzania 2005 na miss world africa NANCY SUMARI ambae kwa mara ya kwanza amefanya uzinduzi wa kitabu chake cha NYOTA NJEMA ambacho kwa maelezo yake amesema kinalenga kumpa  mtoto changamoto ya kujikubali akiwa bado mdogo.


Hapa akiwa katika studio za CLOUDS AKIFANYA MAHOJIANO NA dinna marios wa LEO TENA












Tuesday, March 19, 2013

Yesuuu Nakupendaaa'

''Yeeeesuuuuuu'''nakupendaaaaaaaa''
''U mali yangu,umebaki pekee kwangu''
''kaa nami siku zooteeeeeeeee''

Hakika ni neema ya ajabu kuwa na ulinzi mkuu kutoka kwako,niseme nini mbele zako MUNGU wangu kwani ukuu wako ni wa ajabu maishani mwangu..
Wapendwa nina kila sababu ya kumshukuru mungu kwani kwa mara ingine amenionekania na kujidhihirisha kwani naamini Bwana wetu hatotupungukia na tukimwita yeye hutujibu..

Ninachojifunza ni kuwa dears tusikate tamaa na majaribu ni mtaji wa kupandisha imani zetu,kwa eneo ulilopo  amini Mungu anajua hitaji lako na atafanya tu no matter ni majaribu gani unayapitia sasa'''Yeye ni jina lipitalo majina yote'''amini tu usikatishwe tamaa na jaribu ulilonalo

barikiwa rafiki''

Sunday, March 17, 2013

NI KWA NEEMA TU''

Mpendwa umewahi kujiuliza ni kwa jinsi gani MUNGU wetu ni wa upendo juu ya maisha yako?Je  ni wangapi wana matatizo makubwa zaidi yako au labda ni vipi imetokea kuona wewe ni bora zaidi ya wengine na kujiona yote unayofanya ni kwaajili ya utashi wako binafsi?? Nilikua nikisikiliza wimbo huu asubuhi ya leo na kutafakari ukuu wake...HAKIKA WOTE TUNAISHI KWA NEEMA TU si kwamba sisi ni bora kuliko wengine,sifa na shukrani ni kwako Mungu wetu......


Ni jumatatu nzuri nawatakia jumatatu njema na Mungu awaongoze'''



Wednesday, March 13, 2013

HAYA NI MAPITO TU


EEEHHH' MUNGU tusaidieeee''

Siku hizi binadam tumekuwa kama wanyama NA ni afadhali na mara mia ya wanyama na hatuoni thamani tulizonazo hata kufanya yasiyostahili....Hii ni habari ya mda kdg ila katika pitapita zangu kuna rafiki yangu wa karibu alinipa hii ''case'' ya huyu dada jamani kwakweli binadam wa sasa ni wachache wenye huruma na utu.....kweli wapo ila sio wote ni wachache mnooooo,jamani mnooooo'''mh''nilishindwa kuvumilia chozi likanitoka

 

Kwa wewe ambae hukuona ilikua hivi,,,,

undefined

                                                            Sophia rashid
“HAYA ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si kazi ya binadamu, nasikitika kwa sababu mume wangu amenitelekeza baada ya kuona watoto wamevimba kichwa,” hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sophia Rashid , 22, mkazi wa Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambaye anauguza wanaye wawili wanaosumbuliwa na uvimbe wa kichwa.

Mama huyo alisema watoto wake hao aliwazaa wakiwa na matatizo ya kuvimba vichwa kutokana na kujaa maji, hali ambayo inamfanya akose raha.

“Kwangu sasa imekuwa ni matatizo makubwa mwanangu Omari mwenye miaka minne na Maulid mwenye miezi kumi wanasumbuliwa na ugonjwa mmoja ambao umesababisha baba yao kuwakimbia,” alisema mama huyo akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi)…
Aliongeza kuwa, tangu alipofika hospitalini hapo wiki mbili zilizopita, amekuwa akipata msaada kutoka kwa maofisa wa ustawi wa jamii wa Moi lakini ndugu zake hawafiki kabisa kumjulia hali.
Daktari mmoja hospitalini hapo aliyezungumza kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini alisema kuwa, hali hiyo huwapata watoto kutokana na kuwa na upungufu wa madini ya pholic acid na mjamzito kukosa lishe bora wakati wa ujauzito.
MSAADA
Kutokana na matatizo hayo mama huyo anaomba kusaidiwa na mtu yeyote aliyeguswa na masaibu yake kifedha, chakula, mavazi, dawa pamoja na kipimo cha TC Scan ambacho alidai kuwa kipo katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam na gharama yake ni shilingi 258,000 kwa mtoto mmoja.
Atakayependa kumsaidia mama huyo atumie simu namba 0716755384 au afike Hospitali ya Muhimbili, Moi kwenye wodi A.

  HUU ni msalaba wa mwenzetu Sophia ila kiuhalisia wote tunapaswa kuona ugumu alionao'Hii ni pesa ndogo ambayo kwa mtu na uwezo wake anaweza fanya bila hata kuwaza au kufikiria mara mbili jamani ......Ni  jukumu la wenye nacho au wasionacho kusaidia kwa nafasi yoyote mtu unaweza msaidia mwanamke mwenzetu Na MUNGU atakuongezea kwa ulichotoa coz naamini kuna watu kama hawa sehem fulani wanahitaji kusikia japo neno la faraja tu hawalipati so nahisi tunaweza fanya kitu kwaajili yake.

  

 '''SAD NEWS'''

NILIFANYA JITIHADA ZA KUMTAFUTA 

Nilifanikiwa kumpata na habari ya kusikitisha ambayo niliyokutana nayo aliniambia tayari watoto hawa wamefariki dunia na hata arobaini yao bado na msiba ulikua nyumbani kwao chanika.......iliniuma na kusema bado Mungu anapaswa ashukuriwe kwa kila jambo yeye ana makusudi juu ya maisha ya sophia kama ilivyo kwangu na kwako.'Bwana ametoa,bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe''

 

MUHIMU

Sihitaji kupokea pesa yoyote ila tutachokifanya kila mtu kwa nafasi yake au km group kwa wale watakaokua tayari kusaidia kupanga siku tukapata mda mfupi tu  tukamtembelee na itategemea tutakavyoamua na kumtia moyo'au unaweza kuwasiliana nae na kujua vp unaweza kumfikia na kumpatia pole yako kwa matatizo haya yaliyompata.

    

Huyu dada alitoa namba yake hapo juu na NAWIWA KUSEMA binafsi nahisi kufanya chochote kidogo kwa ajili yake hata kama ni kidogo,kama unatamani kuungana na mm ktk hili tuwasiliane na tujue nn cha kufanya ili tujitoe kwa ajili yake hata kidogo,,,,nasisitiza hata kidogo usijidharau amini wewe ni msaada wa mtu fulani mahali popote ulipo sio lazima pesa ni chochote........TUWASILIANE KWA

 0714 950054,0754207238 au bkanemba@yahoo.com

   

MUNGU AKUBARIKI SANA''

                   




Saturday, March 9, 2013

HAAAAA''JUST IN PART 1.!!!!! inspirational for our kids



Nilipoiona hii kwa mara ya kwanza i was like uuuuuuuuh''' hawa watoto jamani ni talented na sisi kibongobongo tunaweza kujua pia ni nn mtoto wako yuko ''so in'' nacho na kupalilia eneo hili la kipaji.......
Nitaendelea kukuletea vijimambo vyao tupate kujifunza na kuinjoy ha haaaaaa.......


  

Na hapa je''''''



Tuesday, March 5, 2013

KONA YA MAPOCHOPOCHO'''by NANZA MBUJI

     Wadau ni kipengele kipya katika blogu yangu ambapo nitakua nikikuletea mapishi mbalimbali na kwa pamoja tunaweza kubadilishana ujuzi katika eneo hili la jikoni. Tunajua watu tuna ujuzi mwingi jikoni na kutokana na hilo basi tusiwe wachoyo kushirikiana katika kijieneo hiki ha haaaaaaaa'''.
Kupitia hapa nakukaribisha wewe mdau wangu unitumie aina la pishi uliloamua kutufundisha  katika eneo lolote yaweza kuwa ni vyakula vya kawaida vya watu wazima,matayarisho ya juyce mbalimbali,vyakula vya watoto,refreshments etc na tutaiweka hewani kwa faida ya wote,
tuma kupitia bkanemba@yahoo.com au tuwasiliane kwa 0714950054 na tutajie na jina kamili au ukipenda tupia na picha yako tujue nani aliyetuandalia,khaaaaa hii ni wonderfull

 

 PISHI LA MCHUZI WA KUKU WA NAZI NA MAYAI YA KUCHEMSHA







Vipimo
Kuku 2 Lb (ratili)
Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai
Ndimu 1 kamua maji
Chumvi kiasi
Bizari manjano ½ kijiko cha chai
Vitunguu maji 1
Nyanya 2
Tuwi la nazi zito 1 ½ kikombe
Mayai ya kuchemsha 6

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Mchemshe kuku na tangawizi na ndimu na chumvi mpaka akauke.
  2. Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika mashine (blender).
  3. Mimina kwenye kuku pamoja na bizari zote.
  4. Acha achemke kisha tia tui lichemke mpaka liwe zito
  5. Tia mayai ya kuchemsha.
  6. Pakua kwenye bakuli tayari kuliwa na wali au mkate 
   Shukrani za pekee zimwendee 
       Wa ukweeeel'''nanza mbuji
              BIG UP kwako na tunasubiri mambo mazuri   zaidi toka kwako.

 WADAU,kaeni mkao wa kula next tym ntapost picha zake,stay tuned''''
                                         
                   '' KHAAAAAAA'HAPANA CHEZEA YEYE''