Thursday, December 20, 2012

ANGELA CHIBALONZA


Sifa na utukufu ni kwa Mungu wetu aliye hai! 

 Neno la Mungu linasema, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; uendapo katika moto hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.(Isaya 43:1b-2). 

Mpendwa kumbuka Mungu aliyekukomboa alikuahidi kuwa atakuwa pamoja nawe wakati wote, kumbuka pia Mungu si mwanadamu hata aseme uongo. Simama imara ukiliitia jina la Bwana, songa mbele ukimtumikia na kumtumainia hakika hatma yako njema ya ushindi inakuja. Kwa maana Bwana anasema “…Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia INGOJEE kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia!(Hab.2:2-3). 

       Usikate tamaa mpendwa, kumbuka ahadi za Bwana juu ya hali unayopitia, kiri ushindi kwa kuwa wewe ni mshindi! unajua kwa nini…!unayemtegemea, Bwana Yesu alishashinda pale msalabani!usife moyo, songa mbele. Mungu akubariki.

   Hakika Mungu yeye anaishi  na kamwe hapungukiwi,ni angela chibalonza na wimbo wake WA yahwe uhimidiwe,
Please sikiliza huu wimbo na utafakari

No comments: