Monday, December 31, 2012

foods stands



Jamani nani kasema vyakula havifanyiwi design?????

Chakula kina umuhimu wake kwenye miili yetu, sasa basi sio kupika tu vizuri, bali hata kukiandaa vizuri kwa kula, eidha mezani, etc. Tuna jua kuna hotpots, lakini inabidi ubunifu pia, nimezifuma hizi stand za chakula,

 kwakweli ukiziweka mezani hata kama huna appetite itakuja wandugu. Hii bei yake ni  Tshs. 35,000/= ya kwanza na ya pili(hizi stand ni bila sahani, na sahani zapatikana dukani kwangu na kama unazo zako inafaa pia leta sample tutakutengenezea)

Hii ni 45,000/= na ya juu hapo ni 60000=




Sunday, December 30, 2012

KID's beds designs PARTY 4


Tuliweka pazia, chumba chao kina madirisha 2....watoto ni wa kiume.....miaka yao ni wa kwanza ana 2 yrs. na wa pili ana miezi   3 sasa....



Kitanda hiki ni cha mtoto wa miezi 3, tulimuewekea hizi chuma pembeni ili kuzuia asidondoke....



vitanda vinavyoonekana kwa mbali......magodoro yatawekwa na yeye mteja, alikua hajanunua bado...

  Pazia kwa mbali na vitanda.... chumba kilipendeza .....

 

MWAKA 2013!!!!!!!! RUHUSU AMANI YAKE KATAA MAHANGAIKO


Yamebaki masaa machache mpaka kuuona mwaka 2013'''''

Jamani Mungu ana huruma, wema,neema,rehema,upendo sana,

ukitafakari unaweza anza kulia tu hata kama ni mwanaume na haijalishi uwe ofisini,maombini, unaendesha gari,umelala,unatembea, unapika,unasoma, unalima huko village, uko bafuni unakoga, unaweza piga magoti huko huko hata haisumbui, maji ya mvua uyayokoga yanapoendelea kukumiminikia, unaweza anza kububujika na machozi ya furaha na kunena mara tu ukumbukapo wema  na fadhili zake............


Usikate tamaa kwa yale ambayo hayakuwezekana 2012 basi amini kuwa yatafanyika kwa uwezo wake,.....

blogu hii ya burudika inawatakia kila la kheri katika maandalizi ya kuukaribisha mwaka 2013!!!!

WE ALL LOVE UUUUU!!!!!!

 

 

WANAMUZIKI WA INJILI NA WACHEZA FILAM WAKIWA NA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO

Ni kikao kikubwa kati ya wadau na viongozi mbalimbali wa muziki na filamu na Mheshimiwa Makala ambaye ni Naibu waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo

Lengo la kikao hicho ni wasanii kufahamishwa jinsi serikali ilivyojipanga kuwasaidia wasanii wa Tanzania, ili wanufaike na kazi zao na kuwajengea heshima zaidi.

Katika kikao hicho chama cha muziki wa Injili Kimewakilishwa na  Addo November, John Shabani, Bahati Bukuku, Upendo Kilahiro, Cosmas Chidumule, George Mpella na Stella Joel,pichani ni matukio katika kikao hicho




              Bahati bukuku akiongea jambo wakati wa kikao


        Hapa wadau wakipata picha ya pamoja wakati wa kikao hicho


            Pichani ni mcheza filamu maarufu JB akichangia hoja na mawazo yake

        



            Ni mcheza filamu Ray akiongea na waziri wakati wa kikao hicho

Friday, December 28, 2012

OH''APPRECIATION''


OFFICIALLY!!!!!!!!
INTRODUCING TO YOU,
 THE SPONSORSHIP OF MY BLOG FROM 

HOMEZ DECO
creative Homez


Homez Deco -  Kreative Homez

Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani
 zangu za dhati na za pekee zimuendee mmiliki wa HOME DECO Sylivia a.k.a mama jaydan kwa kunipa fursa ya udhamini wake kuendesha blogu yangu .Si kwamba ninafaa sana ila ni neema ya Mungu kumshukuru kwa kila hatua anayokupa katika maisha,nina furaha ya ajabu katika hili!!

Namshukuru Mungu kwani nahisi ni hatua ingine ambayo amenipa kwa mwaka 2013.Napenda kuwafahamisha rasmi kuwa kuanzia sasa wadau wangu mtakua mnapata vitu mbalimbali kwa bei za kawaida kabisa ambavyo vinapatikana homez deco na utaweza kutoa oda yako na tutakufikia hapo ulipo.Nitafute kwa chochote utakachopenda na tufanye kupitia no.0714950054,0754207238 

beatrice AU kwa e-mail yangu bkanemba@yahoo.com

Tunakukaribisha kwa jinsi ya pekee sababu tunaamini bila wewe mdau hatuwezi kufanya chochote...TUNAKUTHAMINI na KUKUPENDA.jisikie huru kutoa maoni,mawazo yoyote ya kujenga na kukosoa sababu tunaamini mtu huwezi kujifunza bila kukosolewa.


Guys feel at home,

lets decorate..... 
u a most wellcome@'''''










Thursday, December 27, 2012

YOU MUST WATCH THIS GUYS''

HAKIKA MUNGU WANGU WEWE NI MKUU........

Maneno ya kusema yameniisha ila kilasiku nitakusifu na kukuhimidi na kuliinua jina lako juu



IRENE UWOYA ASHEHEREKEA BIRTHDAY YAKE NA WAGONJWA MWANANYAMALA

Tumezoea kuona tofaoti kwa baadhi ya mastaa mbalimbali kufanya party kubwa na nzuri katika kusherehekea siku zao za kuzaliwa, hivi karibuni Irene Uwoya aliamua kufanya kitu tofauti katika siku yake ya kuzaliwa, December 18.

Muigizaji huyo mrembo aliamua kwenda kwenye hospitali ya Mwananyamala kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa ikiwa ni pamoja na kuwafariji.

 

Ilikua kama ifuatavyo katika pichambalimbali........kwa uhakika lilikua wazo zuri na huu ni mfano wa kuigwa 
































Wednesday, December 26, 2012

BARNABA NA SUMALEE LONDON

Ni katika sherehe za kesheherekea miaka 51 ya uhuru wa Tanzania bara........

Matukio katika picha yalikua hivi,





Ni naibu balozi akizungumza katika onyesho hilo

 Ni Mc Gestina George akiwa na safina kassu



Ni gestina akifanya utambulisho mbalimbali




Sunday, December 23, 2012

CREATIVITY OF CHRISTMAS


Christmas Tree


Ni creativity ambayo sikuwahi kuiwaza jamani but ni zaidi ya Maandalizi sababu ni Matairi ya gari ambayo katika hali ya kawaida huwezi kutarajia.

Haya ni matairi na mchanganyiko wa vifaa vingine vya magari then akaweka mapambo kupata muonekano wa mapambo katika kuonyesha maandalizi ya sikukuu hii ya christmass

hakika aliyebuni hii kitu anatakiwa kupata pongezi 


UONGOZI WA BURUDIKA Unawatakia maandalizi mema ya sikukuu ya CHRISTMASS na maandalizi ya kuukaribisha MWAKA MPYA


Tcheeeeerssssssss'''''




















Friday, December 21, 2012

ALIYEDHANIWA AMEKUFA AFUNGA NDOA KANISANI

YAHWE UHIMIDIWE!!!!!!!!!! 
 Uaminifu wako umejulikanaaaaaaaa'''''''''
Kwa mataifa yote ya ulimwenguuu'''''''''
Yahweeeeeeee eeeeeeeee''''''''''''

Hakika shetani imekula kwake..........ilikua ni kwamba asiione siku yake inayofuata ila Mungu aliweza kujidhihirisha   miongoni mwa nguvu za giza...JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akimvisha pete mkewe Magreth Mtebe huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru Mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Jumamosi.







Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi Emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100  Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia Jumamosi mida ya saa sita na nusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndipo ajali hiyo ikatokea maeneo ya Mafiati Mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo.














Tuna kila sababu ya kukiri kuwa shetani ameshindwa na hana mamlaka katika ufalme wa Roho mtakatifu








NANI MSHAMBA YA STARA THOMAS

  STARA THOMAS.............                     


 Ni Aliyekua muimbaji wa nyimbo za bongo fleva Stara Thomas sasa amempa Bwana Yesu maisha yake!
 

Hapo awali alisikika kwa nyimbo maarufu kama Sikia, Sitorudi nyuma, my body na Chldren rights ambapo hivi karibuni amevuma na wimbo wa nipigie alioshirikishwa na AT.
 

Stara alipoulizwa kuhusu  maamuzi yake haya binafsi alieleza 

“Nilipata wito kutoka kwa Yesu kwa kuwa aliwaita watu wote wasumbukao na kulemewa na mizigo waende kwake atawapumzisha” alisema.


Awali alikua akiabudu dhehebu la Jamatrine kwa sasa anaabudu kanisa la Shalom lililoko Mbezi Salasala! NA endapo ukihitaji kumuunga mkono kwa kununua album yake mpigie simu ifuatayo +255 718 030 411


    Uongozi wa BURUDIKA BLOG UNAKUTAKIA KILA LA KHERI NA MUNGU AKUBARIKI katika kulitangaza jina la bwana


Hii ni cover ya Albamu yake hiyo mpya kama inavyojieleza
hapa ikionyesha nyimbo zilizomo katika albam hiyo
                    



VIONGOZI WA CHAMA CHA INJILI WAPATIKANA RASMI

Ni katika  Hotel ya Wanyama iliyoko Sinza Mori kumefanyika kongamano la waimbaji wa Muziki wa Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania "CHAMUTA" 
 limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania.

Katika kongamano hilo lilihudhuriwa na Mfuko wa pensheni wa LAPF.Mfuko huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae,pia kutoa fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.  

Pichani ni baadhi ya matukio katika kongamano hilo


Mwanamuziki mkongwe wa injili UPENDO KILAHIRO akiongea katika kongamano hilo katika Hoteli ya wanyama sinza


Mwimbaji wa muziki wa injili BAHATI BUKUKU akisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo



                           Mwimbaji mkongwe nchini mzee Makasy akiandika point muhimu

               Pastor Abel Orgenes ambaye amekuwa karibu sana na waimbaji wa gospel


                 Comedian King Chavala alikuwepo kujua umuhimu wa chama hicho

 Hapa ni mwimbaji maarufu Addo November Mwasongwe Rais wa chama cha wasanii akiwa na mkurugenzi wa Grace Product.

PICHANI CHINI............

           Abubakar Ndwaka meneja mafao wa LAPF akizungumza jambo katikakongamano hilo