AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEA MWANADAMU
Nguzo ya siku'''''''
IMANI YAKO ikimgusa MUNGU hautabaki kama ulivyo
Leo nawakumbusha wapendwa kuhusu kumtegemea MUNGU, na kumtumaini yeye
kama BWANA NA MWOKOZI
(ISAYA51;7)Amebarikiwa mtu yule amtumainiye BWANA,
kwa maana hiyo kuna baraka katika kumtumaini BWANA, lakini kuna laana
katika kumtumaini mwanadamu kama kinga(ISAYA51;5),
Usimtumaini mwanadamu
MUNGU hapendi wewe umpe utukufu mwanadamu, hebu litaje jina la BWANA
kila wakati, usitaje mali uliyonayo haitakusaidia(ZABURI 20;7) hawa
wanataja farasi na hawa magari lakini sisi tutalitaja jina la BWANA.Hata
kama unataka pesa hebu litaje jina la BWANA kwani amesema pesa na
dhahabu ni za BWANA(HAGAI 2;8)
No comments:
Post a Comment