UNGANA NA MCHUNGAJI KANEMBA KATIKA MAOMBI YA DUNIA
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni ambaye yuko South afrika
Kwa masomo, ameanzisha mtandao wa maombi kwa njia ya skype. maombi hayo
ambayo yameanza mwezi uliopita yamekuwa ya baraka sana kwa wanaoshiriki.
akiongea kutoka UK Bonny Shauri amefurahi jinsi technolojia
inavyowezesha watu kutoka pande tofauti za Dunia kufanya maombi ya
pamoja, maombi hayo yanayoongozwa na mchungaji huyo yanalenga sana
mahitaji muhimu ya kila siku kama ifuatavyo
1. Afya
2. Taifa (Serikali)
3. Kanisa
4. Uamsho
5. Mafaniko kiuchumi na baraka za ndoa na watoto
kwa sasa ambao wameweza kujiunga na mtandao huu wa maombi ya live ni
Familia ya Silomba iliyoko Marekani, Familia ya Bonny Shauri Iliyopo UK,
Ndugu Japhet aliyeko Sweden, Martin Malecela Tazania, Issack Kisiva
Tanzania, Joseph Mwakibuti Tanzania, Peace Lumelezi na Charles Mwaihojo
Tanzania na yanaongozwa na mch akiwa south Africa. maombi hayo ambayo
yanafanyika kila jumamosi usiku kuanzia saa 22:00 kwa saa za Tanzania.
Mchungaji Kanemba ameomba watu mbalimbali kujiunga ili tuweze kuomba kwa
pamoja maana ni njia mojawapo ya kusababisha mafanikio katika familia
zetu, maombi hayo ambayo huanza na neno linalotolewa na mch halafu
maombi na kama kuna mtu mwenye hitaji binafsi basi baada ya maombi
anaweza kuwasiliana na Mch kwa maombi na ushauri zaidi kwa njia hiyo ya
skype.
hakika hakuna linaloshindikana mbele zake mungu...katika umbali wowote mungu anafika na kukujibu haja ya moyo wako
No comments:
Post a Comment