Baada ya kukaa nje ya kwaya yake kwa takribani miaka miwili sasa, hatimaye malkia wa kundi la Ambassadors of Christ wana ''Kwetu Pazuri'' kutoka kanisa la kisabato Remera Rwanda, Umulisa Yvonne Habimana, amerejea rasmi katika kwaya yake na kuwa endapo mahudhurio yake yatakuwa mazuri anategemea kuwemo katika album mpya ya kwaya hiyo ambayo wanatarajia kurekodi karibuni.
Yvonne ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza mapema mwezi wa tano mwaka huu nakumpa jina la Aria Tesi kwa muda wote huo amekuwa nje ya kwaya hiyo na kufanya mashabiki wake na wa kwaya hiyo kuulizia uwepo wake popote kundi hilo hata wimbo maarufu uliolitambulisha kundi hilo wa ''kwetu pazuri'' aliouimbisha mwanadada huyo kuanzishwa na mwanadada mwingine aitwaye Sarah Uwera.
Yvonne na mtotowake Aria Tesi Habimana.
No comments:
Post a Comment